facebook likes

Monday, September 2, 2013

OZIL MBIONI KUJIUNGA NA ARSENAL KWA ADA YA UHAMISHO WA £42M KUTOKA REAL MADRID

Klabu ya Arsenal iko mbioni kukamisha usajili wa kiungo wa Real Madrid Mesut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili barani ulaya.
soma zaidi...........
Kwa mujibu wa ripoti zilizoenea mitandaoni ni kwamba Arsenal wapo katika mazungumzo ya mwisho na Real Madrid juu ya usajili wa Ozil .

Kiungo huyo wa kijerumani mwenye miaka 24 amekuwa Bernabeu tangu mwaka 2010 akitokea Werder Bremen.
Na Ozil anaweza kuelekea Emirates Stadium baada ya Gareth Bale kujiunga rasmi na miamba ya soka la Hispania akitokea Tottenham kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya £85.3m.
Ozil ameshaitumikia Madrid katika michezo zaidi ya 100 huku akiwa na rekodi ya kuongoza kwa assists nyingi zaidi barani ulaya katika misimu mitatu iliyopita. 

Gunners wapo karibu kukamilisha usajili wake wenye thamani ya  £42.5m, lakini bado watapambana na upinzani mkali kutoka kwa 
Manchester United na Paris Saint Germain ambao pia wamehusishwa na mchezaji huyo. 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...