facebook likes

Thursday, September 5, 2013

Mbali Na Kipaji Kikubwa Mvuto Na Nafasi Aliyokuwa Nayo Katika Muziki, Huyu Ndiyo Star Wa Muziki Ambaye Kwa Muda Mrefu Alikuwa Hajiamini Juu Ya Uwezo Wake Wa Kuimba

Mbali na mafanikio makubwa aliyonayo kimuziki, Jennifer Lopez amewashangaza wengi hasa baada ya kuweka wazi kuwa amekuwa kwa muda mrefu sana na tatizo la kutokujiamini katika uimbaji wake.
SOMA ZAIDI...................Msanii huyu amesema kuwa, kutokana na shida hii, alifikia hadi hatua ya kujiona kuwa, yeye sio mzuri katika kuimba kwa kiasi ambacho watu wanamchukulia, na kujiamini kwake kulikuja mara tu baada ya kujifungua watoto wake mapacha [Max na Emme].
Jennifer ameweka wazi kuwa, Aliyekuwa Mume wake na Baba watoto wake Marc Anthony ndiye aliyemsanidia kwa kiasi kikubwa kumpa moyo na kumjengea kujiamini yeye na sauti yake na kumuwezesha kusonga mbele.

Jennifer amesema kwa sasa ameweza kujitambua na kujiamini katika kile anachokifanya.

Mbali na tatizo hili kubwa alilokuwa nalo, Jennifer amefikia hadi hatua ya kuwa jaji wa mashindano makubwa sana ya kusaka vipaji vya kuimba ya American Idol, ambapo atakuwa jaji katika mashindano hayo kwa msimu mwingine tena.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...