facebook likes

Thursday, September 5, 2013

Huyu Ndiye Star Wa Rap Aliyeingia Katika Scandal Ya Kuazima Madini, Anadaiwa Zaidi Ya Shilingi Milioni 161 Baada Ya Kutoweka Nayo Moja Kwa Moja

Staa wa muziki kutoka mbele, Tyga ameingia katika 'skandali' kubwa  ya kesi ya madai ya fidia baada ya kile kinachosemekana kuwa ni deni la kiasi cha dola zipatazo 100,000 ambazo anadaiwa kwa kuchukua/kuazima vito vya thamani ikiwepo chain na saa za almasi katika duka bila kulipia.
                      

SOMA ZAIDI............Mdai wa raopa huyu ni Jason kutoka Beverly Hills Jewerly ambaye anasema kuwa msanii huyu, mwaka jana mwezi August alichukua saa yenye nakshi za almasi na kuahidi kulipia kiasi cha dola 28275, na pia baadaye aliazima cheni ya dhahabu ya thamani ya dola zaidi ya 91000 na mpaka sasa hajaweza kurudisha na wala kulipia madini haya.

Story hii imemshushia hadhi kwa kiasi kikubwa msanii huyu ambapo kwa sasa imefahamika kuwa, kwa sehemu kubwa madini [bling bling] anazotupia, huwa anaziazima na si  mali yake kama wengi wanavyofikiri.

Deni la msanii huyu kwa bei ya kueleweka kibongo ni zaidi ya shilingi milioni 161.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...