Ni miaka 17 imepita toka legend wa Hip hop
Tupac Amaru Shakur afariki dunia (September 1996) lakini kazi zake
alizozifanya kipindi cha uhai wake zinaendelea kuingiza pesa kutokana na
mirahaba ya kazi hizo.
Tupac na mama yake Afeni enzi za uhai wake
SOMA ZAIDI.....
Mama yake mzazi na Tupac Shakur amefungua
kesi ya kudai kiasi cha dola milioni 1. 1 za mrahaba (royalties) kutoka
katika albam iliyotolewa baada ya kifo cha rapa huyo aliyefariki (1996).
Afeni Shakur mwenye miaka 66 amefungua kesi
hiyo dhidi ya kampuni ya Entertainment One kwa madai ya kampuni hiyo
kuvunja masharti ya mkataba kwa kushindwa kulipa mirahaba ya album ya
Tupac “Beginnings: The Lost Tapes,” ambayo ilitoka (2007).
Kampuni ya E1 ilinunua haki za muziki wa Tupac kutoka kwa Death Row Records iliyofilisika (2006) kwa mujibu wa mashtaka hayo.
Afeni ni ‘Co-administrator’ wa kazi za
mwanae Makaveli ambaye pia katika mashtaka yake amedai kampuni hiyo
irudishe ‘master’ ya kazi zote za Tupac ambazo hazijatoka kwa mujibu wa
ripoti ya TMZ.
Album ya ‘The Lost Tapes’ ina jumla ya nyimbo 10 zikiwemo ambazo Tupac alitoa mwaka (1988).
No comments:
Post a Comment