facebook likes

Thursday, September 26, 2013

Hatimaye beef ya Chris Brown na Drake imemalizika, wana mpango wa kurekodi wimbo wa Pamoja.

Kuna uwezekano ile beef ya staa wa R&B Chris Brown na rapper Drake ikawa imefika ukingoni rasmi baada ya kuonekana wakiwa pamoja na kukumbatiana katika tamasha la muziki la iHeartRadio lililofanyika weekend iliyopita huko Las Vegas, Marekani.

brown_drake SOMA ZAIDI.....


Breezy na Drizzy hawakuwa katika wakati mzuri toka tukio la kurushiana chupa katika night club ya New York mwaka jana (2012) na baadaye kukawa na mvutano juu ya mapenzi ya Rihanna ambaye pia amewahi kuwa mpenzi wa Breezy.
Kwa mujibu wa chanzo, Katika tamasha hilo la iHeartRadio Drake na Breezy walionekana wakipiga story na kukumbatiana backstage huku wakipata vinywaji.Taarifa hiyo zinaongeza kuwa Drake alikuja na kundi la washkaji zake maalum kabisa kwaajili ya kutazama performance ya Breezy.
Kikubwa zaidi katika kumaliza wingu lililokuwepo kati yao, wawili hao wana mpango wa kuingia studio na kufanya wimbo wa pamoja, kwa mujibu wa chanzo kilichouambia mtandao wa Page Six.
Upande wa kazi zao filamu mpya ya ya kudance ya Chris Brown ‘Battle of the year’ imeingia katika theatres September 20, wakati album mpya ya Drake ‘Nothing Was The Same’ imetoka rasmi jana (September 24).

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...