facebook likes

Thursday, August 29, 2013

NEYMAR ATWAA TAJI LA KWANZA BARCA

barca 9e8c3

Bao la Neymar katika mechi ya kwanza limempa taji la kwanza Barcelona (HM)
Barcelona wamesherehekea rekodi ya kutwaa Super Cup ya 11 Hispania dhidi ya Atletico Madrid
SOMA ZAIDI.............
barca2 b779a

NYOTA wa Brazil, Neymar ameshinda taji lake la kwanza Barcelona kufuatia vigogo hao wa Katalunya kutwaa taji la nne la Super Cup ya Hispania ndani ya miaka mitano kwa faida ya bao la ugenini, baada ya sare bila kufungana 0-0 usiku wa jana Uwanja wa Nou Camp.
Baada ya sare ya 1-1 wiki iliyopita Uwanja wa Calderon, bao la Barca likifungwa na Neymar, aliyetokea benchi kuisawazishia timu hiyo mjini Madrid, alianzishwa katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo majira haya ya joto akitokea Santos ya kwao.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi pia alirejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi, lakini wote walishindwa kutikisa nyavu za wageni.
Messi alikosa hadi penalti baada ya kugongesha mwamba na mpira ukarejea uwanjani.
Katika mchezo huo, wachezaji wawili walitolewa nje kwa kadi nyekundu, Filipe Kasmirski dakika ya 80 na Arda Turan dakika ya 90 na ushei.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Victor Valdes, Dani Alves, Gerard Pique, Javier Mascherano, Jordi Alba, Sergio Busquets, Xavi, Cesc Fabregas/Andres Iniesta dk73, Alexis Sanchez/Pedro dk65, Neymar na Lionel Messi.Atletico Madrid: Thibaut Courtois, Miranda, Diego Godin, Luis Filipe, Juanfran, Gabi, Koke/Leo Baptistao dk89, Mario Suarez, Arda Turan/Adrian dk72, Diego Costa, David Villa/Cristian Rodriguez dk84. 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...