facebook likes

Thursday, July 4, 2013

Kuhusu usajili wa Gonzalo Higuain kwenda Arsenal

Usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina kuelekea klabu ya washika Bunduki wa Huko London kwenye uwanja wa Emirates Arsenal utakamilika hivi karibuni kwa mujibu wa baba yake mzazi pamoja na kaka yake ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo . Jorge Higuain amesema kuwa mwanaye atakuwa mchezaji wa Arsenal ndani ya siku chache zijazo baada ya kupata ruhusu toka kwa Real Madrid ya kuzungumza rasmi na Arsenal .
Taarifa zaidi ambazo zimethibitishwa na wakala wa mchezaji huyo Nicolas Higuain ni kwamba mdogo wake angeweza kuwa amekamilisha usajili wake ndani ya Arsenal tangu wiki iliyopita lakini ilishindika kwa kuwa klabu ya Real Madrid haikuwa imetoa ruhusa kwa wakala kuzungumza na Arsenal . Jorge Higuain kwa upande wake amesema kuwa siku zote hawaweza kufanya makubaliano na klabu nyingine pasipo kupata ruhusa ya klabu anayochezea mtoto wake na ukubali wa Real kutoa ruhusa unamaanisha kuwa Gonzalo atatambulishwa kama mchezaji mpya wa Arsenal ndani ya siku chache zijazo .
Usajili wa Higuain kwenda Arsenal umekuwa ukizungumzwa kwa muda mrefu na baadhi ya mashabiki walikuwa wameanza kukata tamaa hasa ukizingatia ukweli kuwa klabu hiyo imewahi kukaribia kuwasajili wachezaji wengi hapo awali huku mipango ikiharibika mwishoni . Tayari kumekuwa na makubaliano ya msingi baina ya Arsenal na wawakilishi wa Higuain pamoja na makubaliano baina ya Real na wakala wa mchezaji mwenyewe lakini hakukuwa na makubaliano rasmi ya kutoa ruhusa kwa Arsenal kuzungumza na Gonzalo .Gonzalo-Higuain61
Tayari Real Madrid walishaweka wazi azma yao ya kumruhusu mchezaji huyo kuondoka baada ya kuwa ameichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka 6 tangu aliposajiliwa akitokea River Plate ya Argentina .
Gonzalo Higuain mwenyewe ameonekana akiwa kwenye uwanja wa Ndege wa Heathrow huko London ambako inaaminika alikwenda kukamilisha mipango ya awali ya kujiunga na Arsenal ambao wameripotiwa kuwa tayari kuwalipa Real paundi milioni 22 kwa ajili ya mchezaji huyo.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...