Ushindi ilioupata timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano ya
kombe la mabara mwishoni mwa wiki iliyopita umeisaidia timu hiyo kupanda
zaidi ya nafasi kumi kwenye viwango vya ubora vya soka vya FIFA.
Brazil ilianza michuano hiyo ikiwa inashika nafasi ya 22
ambayo ni nafasi ya chini kuwahi kushikiliwa na timu hiyo lakini ushindi
kwenye michezo yake mitano kuanzia hatua ya makundi, nusu fainali na
fainali umeipandisha Brazil hadi kufikia nafasi ya tisa .
Bado Hispania wameendelea kushika nafasi ya kwanza
wakifuatiwa na Ujerumani huku Colombia,Argentina na Uholanzi
zikikamilisha orodha ya timu tano bora za dunia.
Italia ambao walifika hatua ya nusu fainali kwenye kombe la
Mabara wanashika nafasi ya sita mbele ya Ureno walio kwenye nafasi ya
saba huku Croatia , Brazil na Ubelgiji wakishika nafasi za nane, tisa na
kumi .
Timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo mchezo wake wa mwisho wa
kimataifa ulikuwa dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania ambapo Tembo hao
walishinda kwa 4-2 wanabakia kuwa timu inayoshika nafasi ya kwanza kwa
Afrika wakiwa wameshika nafasi ya 13 kwenye viwango vya dunia
wakifuatiwa na Ghana walioko kwenye nafasi ya 24.
Mali ndio timu ya tatu kwa ubora Afrika wakiwa wanawafuatia
na Ghana kwenye nafasi ya 28 huku tano Bora ikikamilishwa na Algeria na
Nigeria wanaoshika nafasi za 4 na 5 wakiwa wameshika nafasi za 34 na 35
kimpangilio kwenye viwango hivyo.
Kwenye ukanda wa CECAFA ambako Tanzania iko ,Uganda wako
kwenye nafasi ya juu wakiwa wanashikilia namba 19 kwa Afrika na 80
kidunia wakifatiwa na Ethiopia walio nafasi ya 25 kwa Bara la Afrika na
nafasi ya 90 Duniani.
Tanzania inashika nafasi ya 35 kwenye orodha ya nchi 54 za Afrika huku ikiwa kwenye nafasi ya 121 Duniani.
No comments:
Post a Comment