Kocha wa zamani wa Bayern Munich Jupp Heynckes amejiondoa kwenye listi ya makocha wanaodhaniwa watapewa kazi ya ukocha wa kuinoa klabu ya FC Barcelona.
Kocha huyo mwenye miaka 68, alishinda makombe matatu na Mabavaria msimu uliopita pamoja kumaliza utawala wa FC Barca kwa kuwapa kipigo cha 7-0 katika mechi mbili za nusu fainali ya klabu bingwa ya dunia, amekuwa akitajwa na vyombo vya habari na mashabiki wa Barcelona kama ndio mtu sahihi kurithi mikoba ya Tito Vilanova, ambaye alijiuzulu kutoka na matatizo ya kiafya.
Lakini, kocha huyo wa zamani wa Real Madrid amejiondoa kwenye listi ya makocha wanaowania jukumu la kuinoa Barca msimu unaokuja na kusisitiza kwamba siku zake za kukaa kwenye bechi la ufundi zimeisha.
"Najiweka bize kwa kufanya vitu vyangu nivipendavyo na kufuatilia michezo. Nina wanyama wangu kwenye bustani," aliiambia Sky Sports News HD. "Nadhani itakuwa haiwezekani kwangu mimi, baada ya kufanya kazi na Bayern Munich, sasa niende kuchukua jukumu kwenye klabu nyingine.
"Nimeelewa ishara za mwili wangu na njihisi nipo vizuri, na nafurahia maisha nje ya soka."

No comments:
Post a Comment