wananchi, wasomaji pamoja na wauzaji wa rejareja wa jarida la Rollingstone, wameshangazwa na kuchukizwa na hata kufikia kusema kuwa ni sawa na kutusiwa na cover jipya la jarida hilo linalotarajiwa kutoka mwezi wa nane, ambalo limepambwa na sura ya kijana aliesababisha mauaji ya Boston Marathon,"Dzhokhar Tsarnaev"
cover hiyo yenye picha nzuuri ya mtuhumiwa huyo ilikuwa na maneno haya.
"THE BOMBER, "How a popular, promising student was failed by his family, fell into radical Islam and became a monster.
malalamiko ya kitendo cha jarida hilo kumpamba muuaji huyo wa mabomu ya boston ambayo yaliua watu watatu, kujeruhi zaidi ya 200 pamoja na ofisa wa polisi mmoja, yalianza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, facebook pamoja na twitter.
Baada ya malalamiko hayo kuenea, maduka maarufu yanayouza majarida hayo yametangaza kugoma kuuza jarida hilo, duka la madawa nchini marekani CVS limetangaza mgomo wa kutokuweka jarida hilo kwa ajili ya kuuza na kuungwa mkono na makampuni mengine makubwa kama Walgreens, duka la glosaries lililopo New England "Stop and Shop", pamoja na Tadesch food shop
kikubwa kinacholalamikiwa ni cover hiyo kuwa na picha ya muuaji wa mabomu, na picha kumuonyesha kama ni innocent na kudai kuwa hakustahili kuwa kwenye cover ya jarida hilo.
licha ya malalaniko hayo, wako waliounga mkono gazeti hilo na kusema kuwa, picha haimaanishi itamfanya muuaji awe ni mtu mzuri, bali kilichoandikwa, na kilichaandikwa na RollingStone ni maisha aliyokuwa akiishi kijana huyo na kilichompelekea mpaka kuwa monster, kitu ambacho ni kizuri kwa watu kuelewa na ni kazi kubwa iliyofanywa na jarida hilo kupata information zote hizo.
No comments:
Post a Comment