Rais mpya wa Iran Hassan Rowhani amesisitiza kuwa nchi yake kamwe haitakua na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na Marekani na nchi za magharibi.
Rais mpya wa Iran Hassan Rowhani
Rais huyo amesema kuwa serikali yake itaelekeza nguvu kwenye mazungumzo na nchi hizo na hivyo kukomesha hatua ya Iran kutengwa na dunia kwa madai kuwa inalenga kutekeleza mpango wa nyuklia utakaozalisha silaha za nyuklia.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Marekani cha NBC, tangu pale alipo chaguliwa kuliongoza taifa la Iran mwanzoni mwa mwezi Agosti, Rohani amethibitisha kuwa alikuwa na mawasiliano na rais Obama ambaye alimuandikia risale.
Katika risala hiyo Rohani amesema Rais Obama alimpongeza baada ya kuchaguliwa kuwa rais kuchukuwa nafasi ya Mahmoud Ahmednejad na kugusia maswali mengine muhimu na ambapo alionyesha kuwa mtulivu.
Rohani ameendelea kusema, alijibu barua hiyo ya Obama na kumshkuru na baadae kumpa maoni ya jamuhuri ya taifa la Iran, mtazamo wangu na risala jiyo ilikuwa na ntazamo ulio chanya na wenye kujenga.
Kauli ya rais huyo inakuja siku chache kabla ya yeye kusafiri kuelekea NewYork Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa umoja wa mataifa huku akiunga mkono msimamo uliotolewa na rais wa Marekani Barack Obama.
Rais Obama amesema ni vema Iran ikapewa nafasi na kujaribiwa kufuatia hatua ya Rais mpya Hassan Rowhani kuonyesha nia ya kufanya mazungumzo ya wazi na nchi za Magharibi na Marekani.
Marekani na Iran zilivunja uhusiano wao wa kidiplomasia tangu mwaka 1979 baada ya mapinduzi
Chanzo - kiswahili.rfi.fr
No comments:
Post a Comment