facebook likes

Wednesday, August 14, 2013

Vijana kutoka Ujerumani wafurahia ushirikiano na Serikali ya Tanzania.


 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza... 
...SOMA ZAIDI.....na vijana kutoka Taasisi ya MitoSt ya Hamburg Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia ushitikiano wao wa kubadilishana rasilimali watu na kujitolea kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition (TYC) walipotembelea Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo wageni hapo wamekuja na ujumbe mahususi wa furaha kwa wote.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana  wanaojitolea kutoka Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia mpango wao wa kubadilishana rasilimali watu kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizarani hapo.
 Afisa Mipango wa MitOst  Mete Odabasi akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kwa niaba ya Wizara ya Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo kufuatia ushirikiano waliopewa katika ziara yao hapa nchini.
 Mmoja wa wanachama wa Tanzania Youth Coalition (TYC) ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bibi Neema Kassala (kushoto) akichangia mada walipokutana na Mkurugenzi wa  Maendeleo yaVijana walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam kufuatia kuwa wenyeji wa wageni kutoka Taasisi ya MitoSt ya jijini Hamburg Ujerumani waliopo nchini.
 Mmoja wa wakilishi kutoka Taasisi ya MitOst yenye makao yake jijini Hamburg Ujerumani Bibi Lusinja Czesnik (wa pili kutoka kushoto) akichangia mada jana walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya kitamaduni kutoka kwa Afisa Mipango wa taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani Mete Odabasi walipokutana na Mkurugenzi huyo  Jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo  jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana na wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza nama Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Frank Shija wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...