facebook likes

Wednesday, August 14, 2013

HOMA YA PAMBANO LA NGAO JUMAMOSI…YANGA WAINGIA KAMBINI JANGWANI CITY, AZAM WAFIKIA COMPLEX


YANGA SC wameingia kambini makao makuu ya klabu yao, Jangwani, Dar es Salaam maarufu kama Jangwani City kujiandaa na mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Jijini.
.....SOMA ZAIDI......
Wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu, wakiingia kambini Jangwani, wapinzani wao Azam FC waliorejea jana kutoka Afrika Kusini walipoweka kambi ya takriban wiki mbili, wamefikia kwenye makao yao makuu, Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umeteka hisia za wengi na kila timu inaonekana kupania kushinda ili kuwasha taa za kijani kuelekea mbio za ubingwa.
Yanga iliifunga Azam FC katika mechi zote tatu za msimu uliopita walizokutana, hivyo kulipa kisasi cha kufungwa na timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa mara nne msimu uliotangulia katika mashindano yote waliyokutana.
Katika kujiandaa na msimu, Yanga SC walicheza mechi saba na kushinda tatu, kufungwa moja na sare tatu.
Walizifunga Mtibwa Sugar 3-1, SC Villa ya Uganda 4-1 na 3Pillars ya Nigeria 1-0, na kutoa sare ya 1-1 na Express, 2-2 na URA zote za Uganda na 0-0 na Rhino FC mjini Tabora, wakati walifungwa 2-1 na Express ya mjini Shinyanga.

Kwa upande wa washindi wa pili wa Ligi Kuu, Azam kabla ya kwenda Afrika Kusini walicheza mechi nne na kushinda tatu, 1-0 na komabini ya JKT, 4-0 na African Lyon na 5-1 Ashanti United. Azam pia ilicheza mechi tatu na kikosi chake cha pili, Azam Akademi na kushinda zote, 1-0 mara mbili na 2-1 mara moja.
Na ikiwa Afrika Kusini, ilicheza mechi nne na kufungwa tatu na kushinda moja- ilifungwa 3-0 na Kaizer Chiefs, 2-1 na Orlando Pirates na 1-0 na Moroka Swallows, wakati yenyewe ilishinda 1-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns. 

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...