Utafiti unaonesha kwamba unywaji wa zaidi ya vikombe 4 vya kahawa kwa
siku unaweza kuchangia hatari ya uwezekano wa vijana wenye umri mdogo kufa
mapema, lakini hii ni kwa wale wa chini ya miaka 55.
....SOMA ZAIDI....
Kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa Marekani unywaji wa vikombe 28 kwa wiki unaongeza uwezekano
wa vifo vya mapema kwa vijana. Utafiti huo uliofanywa kwa maisha ya watu wa
Marekani ulihusisha watu 43,727 wa kuanzia miaka 20 hadi 87.
Mtafiti Steven
Blair, wa University of South Carolina, Marekani amesema matumizi ya kahawa kwa
wingi yanaweza kusababisha athari katika mwili na watu wenye ‘coffee addiction’
ndio wako katika hatari kubwa zaidi.
Hata hivyo
watafiti hao hawakueleza sababu za kwanini kahawa haijaonekana kuwa na madhara
kwa watu wa zaidi ya miaka 55 kama utafiti walivyoonesha kwa vijana. Kahawa ina
kemikali nyingi tofauti ambazo zinaweza kuwa na athari na faida pia kwa afya.
No comments:
Post a Comment