Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania ( Necta), Dk Joyce Ndalichako, ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Serara Moahi wa Botswana..........SOMA ZAIDI.....
Akizungumza baada ya kutangazwa kuteuliwa kwake, Dk Ndalichako alisema atatumia fursa hiyo kuendeleza ajenda mbalimbali zitakazosaidia kuinua elimu Bara la Afrika.
“Hii ni heshima ya pekee kwa Baraza la Mitihani Tanzania, kipindi cha mwaka mmoja nikiwa Rais wa AEAA nitaendeleza yaliyoanzishwa na mtangulizi wangu, pia kutekeleza ajenda mbalimbali zitakazoleta manufaa kwa nchi yetu,” alisema Dk Ndalichako. Pia, alisema atajitahidi kuwa mbunifu na kupanua ushirikiano na nchi nyingine.
, kuhakikisha anawajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa mabaraza ya mitihani kwa nchi wanachama.
“Kwa mfano kwetu naona changamoto kubwa ni suala la standardisation (kusanifisha alama za mitihani), nitajitahidi kuhakikisha watu wetu wanajengewa uwezo kwenye nyanja hii,” alisema.
Alitumia fursa hiyo kushauri nchi za Afrika kuhakikisha zinatilia mkazo zaidi kuongeza walimu wa kutosha, walio bora na vifaa vya kujifunzia. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba, alisema kupata cheo hicho ni heshima kwa nchi.
No comments:
Post a Comment