Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe jana ameanika majina ya watu saba waliohusika kupitisha mabegi
tisa yaliyokuwa na kilo 180 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh8
bilioni,
.....SOMA ZAIDI....
Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja.
Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja.
Alisema mizigo ikishaondoka mikononi mwa
abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa wa Idara ya Usalama wa Taifa,
lakini siku ya tukio hilo mbwa hao walichelewa na walitumika baada ya
mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya chuma.
“Kwa abiria watatu kuwa na mabegi
makubwa tisa yanayofanana si kitu cha kawaida kukwepa jicho la maofisa
wa ushuru wa forodha na vyombo vya usalama, sijui walikuwa wapi siku
hiyo?” alihoji Mwakyembe.
Juzi waziri huyo aliahidi kuyaweka
hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini, na
alitekeleza ahadi hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari,
kusema kuwa watu hao wamenaswa baada ya mfumo wa kamera (CCTV) za uwanja
huo kudaka matukio kadhaa yaliyotokea siku ya tukio hilo, kuanzia saa
9:25 hadi saa 10:30 alfajiri.
Ameagiza wafanyakazi hao wanne pamoja na
askari polisi mwenye cheo cha koplo, mbeba mizigo na mfanyabiashara
aliyekuwa na wasichana wawili waliokamatwa Afrika Kusini, (ambao
hatuwezi kuwataja kutokana na kushindwa kuwapata kujieleza) kuchukuliwa
hatua za kinidhamu, kukamatwa na kuunganishwa na watuhumiwa waliokwenda
na mzigo huo Afrika Kusini.
Mabegi hayo yaliyokuwa na dawa za
kulevya aina ya ‘Crystal Methamphetamine’, yalipitishwa na wasichana
wawili wasanii aliowataja kuwa ni Agnes Gerald ‘Masogange’ na Melisa
Edward ambao walidakwa siku hiyohiyo katika Uwanja wa Ndege wa Oliver
Tambo, Afrika Kusini na tayari wameshafikishwa mahakamani.
Juzi Dk Mwakyembe alifanya ziara JNIA
kukagua utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku tatu baada ya
ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki mbili,
atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika mtandao wa
usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vyote vya
ndege nchini.
Saa nane baada ya ziara hiyo, Maofisa wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wanadaiwa kumkamata Edwin Monyo akiwa na
kete 86 za dawa aina ya heroini na misokoto 34 ya bangi aliyokuwa
akiisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich.
Mpango ulivyosukwa
Alisema siku ya tukio saa 9:28 kamera
hizo za usalama zilimwonyesha mbeba mizigo wa uwanja huo akiwa
anazungukazunguka eneo la kuingilia abiria kama mtu ambaye ana ahadi na
kukutana na mtu fulani.
“Kamera pia zilimnasa ofisa mwingine wa
TAA kwa mara kadhaa akitoka na kuingia ndani ya jengo la abiria huku
akizungumza na simu, kitendo ambacho hakiruhusiwi kabisa kwa wafanyakazi
wa eneo la ukaguzi wa abiria,” alisema na kuongeza;
“Wakati huohuo, kamera zilikuwa
zinamwonyesha askari polisi anayetuhumiwa kuhusika katika mpango huo
akiwa anarandaranda eneo la uhakiki wa hati za kusafiria kama vile
anasubiri kitu fulani.”
No comments:
Post a Comment