Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki
akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Ripoti ya
Uwekezaji ya Dunia ya Mwaka 2013 ambayo imejikita kiundani zaidi
kuangalia muunganiko wa Mahusiano ya Kibiashara na Uwekezaji Duniani.Bi.
Kairuki amesema Tanzania imeweza kupata Uwekezaji mara dufu katika
maeneo ya Mafuta na Utafiti wa Gesi Asilia katika kusukuma pato la
taifa kuongeza ajira na kupambana na umaskini.
Ameongeza
Muunganiko wa Biashara na uwekezaji umepata mwamko mkubwa sana kutoka
kwenye makampuni makubwa duniani na umeleta fursa kwa nchi maskini na
zinazoendelea kama Tanzania kuwa na uhusiano mzuri kiuchumi na nchi
zilizoendelea. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar kwenye ukumbi wa
mikutano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali na mabalozi wakifuatilia uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo ya Uwekezaji Duniani.
Mkuu
wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA akizungumzia
umuhimu wa sera za nchi za Uwekezaji kuhakikisha zinatoa fursa ya ajira
na kupunguza umaskini katika nchini zinazoendelea.
Viongozi wa taasisi mbalimbali, Mabalozi, Waandishi wa habari katika uzinduzi huo.
Mwezashaji
katika uzinduzi wa Ripoti ya Ywekezaji wa Kigeni Duniani ya Mwaka 2013
Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) akiwakaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini
(TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA
kuzindua rasmi ripoti hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa
Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA kwa pamoja wakizindua rasmi
Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013 iliyobeba kauli mbiu
Muunganiko wa Biashara na Uwekezaji Duniani "Global Value Chains".
Sasa imezinduliwa rasmi nchini Tanzania.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda (UNIDO) Emmanuel
Kalenzi akichangia mada baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Uwekezaji Duniani
ya Mwaka 2013.
Kutoka
kushoto Meza kuu ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mifumo ya Teknolojia
kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) John Kyaruzi, Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa
Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA.
Usia
Nkhoma Ledama kutoka Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)
akigawa Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013 kwa wadau
waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mdau akipitia ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi nchini.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment