Mnamo
 tarehe 09/07/2013, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo 
(CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe alitoa kauli kwamba wanaunda kikundi chao 
cha kuwalinda ambacho watakipatia mafunzo ya ukakamavu.
Kitendo
 cha chama chochote cha siasa ikiwemo CHADEMA kuanzisha kikundi cha 
kujihami ni kinyume cha sheria za nchi na endapo watafanya hivyo hatua 
za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kufuatia
 kauli hiyo, Jeshi la Polisi nchini limeanza uchunguzi na litachukua 
hatua kulingana na ushahidi utakaopatikana. Aidha, Jeshi la Polisi 
litamshughulikia mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha sheria bila kujali
 wadhifa wake.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

No comments:
Post a Comment