Imeelezwa
kuwa Jeshi la Polisi na Mahakama bado hawajalichukulia hatua za makusudi
suala la ubakaji watoto ambalo linaonekana likiendelea kuengezeka siku
hadi siku.
Kutolichukulia
hatua huko ni pamoja na adhabu ndogo wanazo pewa wahalifu na
kutoridhishwa na ushahidi wa kuona unao tolewa na watu mbali mbali
mahakamani.
Hayo
yamesemwa leo huko katika ukumbi wa Baraza la
wawakilishi chukwani wakati walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara
ya Ustawi wa Jamii ,Vijana Maendeleo ya Wanawake na Watoto juu ya suala
zima la udhalilishaji na ubakaji wa watoto ulivyokithiri hapa nchini.
Wamesema
hali hiyo mbaya inatokana na jeshi hilo na Mahakama
kutochukua hatua za makusudi za kisheria kwa watuhumiwa ambao
wanahusika na kesi za uzalilishaji watoto na na kuwachilia kuwapa
adhabu ndogo au kuto kamilika ushahidi wakuona.
“Polisi
wanataka ushahidi wa aina gani ? kila siku suala la ubakaji
linaongezeka hivi karibuni mtu kafungwa miezi sita kwa kosa la ubakaji
hio ni adhabu ndogo kulingano na kosa lenyewe, alisema mmoja
wawalikilishi hao.
Aidha
walisema kuwa masuala ya udhalilishaji yanafanywa na watu wazima wenye
akili zao timamu jambo ambalo linawasababisha watoto hao kuona
aibu na kuweza kuathirika kisaikolojia .
No comments:
Post a Comment