facebook likes

Friday, July 26, 2013

Anaetajwa kumuoa Genevieve Nnaj mwishoni mwa 2013 ni huyu ‘white’


2 

Kwa mara nyingine tena yule staa wa movie kutoka Nigeria Genevieve Nnaj aliepata sifa ya kutunza siri hasa baada ya kuja kujulikana kwamba alificha siri ya kuwa na mtoto wa kike kwa miaka zaidi ya 15, anamiliki tena vichwa vya habari kwa hili jipya la mume mtarajiwa.
Ni mara nyingi stori zimemuweka kwenye headlines kwamba ataolewa na mwimbaji D’Banj ambae wako mapenzini lakini time hii naambiwa huyu mfanyabiashara raia wa Ghana Mathew Mensah ndio anatarajiwa kumuoa December 2013.
Kuna siku Genevieve aliulizwa kuhusu huyu Mghana ila akaapa kabisa kwamba wao ni marafiki wazuri tu lakini hawako mapenzini kama wengi wanavyoamini, sasa basi stori za kuaminika ni kwamba hawa wawili wanaoana kabla 2013 haijamalizika.
Ni muda mrefu wamekua wakionekana pamoja na inadaiwa hata kwenye birthday ya miaka 33 ya Genevieve huyu Mghana ndio ali-host party.
1

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...