SERIKALI
kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel
na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola
vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.
Taarifa kutoka ndani ya bodi
hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt
aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini
bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya
maadili ya mtanzania.
“Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya
maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka
kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi
hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.
Kabla ya mwandishi wetu hajazungumza
na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa
rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika
mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.
“Amejaribu
kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie mtaani pasipo kuviondoa hivyo
vipande kwani navyo vina umuhimu wake,” alisema rafiki huyo wa Aunt kwa
sharti la kutochorwa jina gazetini.
Alipotafutwa Aunt kuhusiana na
suala hilo, alikiri kukaliwa kooni na bodi na kuomba apewe muda wa siku
mbili ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini hakufanya hivyo,
badala yake akasafiri nje ya nchi.
Mwaka jana mwishoni, bodi hiyo ya
filamu ilimzuia mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ kuingiza sokoni sinema ya
Sister Mary baada ya kuridhishwa na madai ya Kanisa Katoliki
yalioainisha kuwa asilimia kubwa vipande vya sinema hiyo vilidhalilisha
Ukatoliki.
No comments:
Post a Comment