Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akishuhudia mlundikano wa
magodoro na hali ya sehemu wanayolala wavulana wa shule ya Mount Zion
kwenye moja ya vyumba vya darasa vilivyotengwa kwa ajili ya kujisitiri.
ZIARA ya kushitukiza iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina
Masenza akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya
ukaguzi katika shule ya sekondari ya Mount Zion iliyoko ilemela jijini
Mwanza imebaini wanafunzi kuishi katika mazingira hatarishi huku uongozi
wa shule hiyo ukiwaficha vichakani zaidi ya wanafunzi 50 wa bweni
kukwepa ukaguzi.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo taarifa zilizotolewa kwa mkuu huyo na baadhi
ya wasamaria wema hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya na ujumbe wake
kufika shuleni hapo ili kujionea endapo uongozi wa shule hiyo umeboresha
kasoro na mapungufu yaliyoonekana baada ya ukaguzi wa awali kufanyika
kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kutakiwa kuyafanyia kazi
mapungufu hayo na Idara ya Afya na Elimu ukaguzi.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza alishuhudia jinsi hali
mbaya kwa vyoo vilivyounganishwa ndani ya bweni njia zikiwa
zimebananishwa na masanduku ya bati ya kuhifadhia nguo za wanafunzi bila
kuwa na usalama wa kiafya.
Wanafunzi 50 waliobainika kufichwa waumbuliwa.
Hata hivyo jeshi la polisi baada ya kupata taarifa hizo nalo
lilifuatilia na kufanya msako kwenye vichaka vinavyozunguka shule hiyo
na kufanikiwa kuwakuta wanafunzi hao wakiwa wamejificha chini ya ulinzi
wa mmoja kati ya waalimu wa shule hiyo kisha kuwaamuru kwenda shuleni
ambapo mkuu wa wilaya na ujumbe wake walikuwa wakizungumza na uongozi wa
shule na wanafunzi wengine hali iliyo washangaza.
Akizungumza huku machozi yakimbubujika kwa uchungu wa hali aliyoishuhudia shuleni hapo Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza ameeleza kusikitishwa kwa kitendo hicho na kukilaani vikali akiagiza hatua madhubuti za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Mkurugenzi wa shule hiyo…
Akizungumza huku machozi yakimbubujika kwa uchungu wa hali aliyoishuhudia shuleni hapo Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza ameeleza kusikitishwa kwa kitendo hicho na kukilaani vikali akiagiza hatua madhubuti za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Mkurugenzi wa shule hiyo…
Hii ndiyo hali halisi ya ukaaji ndani ya darasa hili jeh kwa mpango huu kuna usalama wa kufanya vyema kazi za darasani na hatimaye kufaulu kwenye mitiani kihalali? |
No comments:
Post a Comment