Stori kutoka London ni kwamba
imefahamika wanigeria wanaoishi nje ya nchi hiyo wametuma nyumbani kiasi
cha dola za kimarekani bilioni 21 mwaka uliopita, kutokana na hilo
Wanigeria hao wameingia kwenye tano bora ya nchi tano ambazo raia wake
wanaongoza kwa kutuma pesa nyumbani.
Nchi ya kwanza ni India, Philippines inafata, ya tatu ni Mexico na ya nne ni Nigeria
Taarifa imeonyesha kwamba India
na China kwa pamoja zimepokea dola za kimarekani bilioni 60 kutoka kwa
raia mbalimbali wa nchi hizo wanaoishi nje ya nchi, Philippines ($24
billion), Mexico ($24 billion), and Nigeria ($21 billion).
Nchi nyingine ambazo zipo
kwenye kumi bora ya raia waishio nje ya nchi kutuma pesa nyumbani ni
pamoja na Egypt iliyoshika nafasi ya 6 ambayo mwaka jana raia wake
walituma nyumbani $18.
Inaaminika ongezeko hilo
limetokana na maisha kuwa magumu ndani ya nchi na raia kutegemea sana
misaada kutoka kwa ndugu zao wanaoishi nje ya nchi pamoja na wanaorudi
nyumbani kwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali hasa ya ujenzi.
No comments:
Post a Comment