Mwandishi wa habari za michezo
Shaffih Dauda ameandika kwenye website yake kwamba miezi kadhaa baada ya
kutemwa na klabu bingwa ya Tanzania bara, Simba Sports Club,
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Danny Mrwanda sasa amepata timu ya
kuichezea huko nchini Vetnam.
Mrwanda ambaye miaka kadhaa
iliyopita alikuwa mchezaji tegemeo wa Simba kabla hajauzwa kwenda nchini
Vetnam kucheza soka la kulipwa katika vilabu vya Dong Tam Long An na
Hoang Anh Gia Lai na baada ya kumaliza mkataba wake akarudi bongo
kujiunga na Simba, lakini muda mfupi baada ya kujiunga na timu akatemwa
kwa madai kwamba kiwango chake kimeshuka.
Akizungumza na mtandao huu
Mrwanda amesema kwamba baada ya kuondoka Bongo, alirudi nchini Vetnam
ambapo sasa ameweza kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya Vetnam klabu ya
DA NANG FC kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
“Nimepata timu huku ya DA NANG
FC, hii timu ndio bingwa wa ligi kuu ya Vetnam. Sasa tutashiriki ligi
ya mabingwa wa bara la Asia.” – Alisema Mrwanda.
No comments:
Post a Comment