Nigeria imepanda kwa nafasi 22
hadi kufika kwenye nafasi ya 30 kwenye viwango vya FIFA vya dunia ikiwa
ni baada ya kufanikiwa kushinda kombe la mataifa ya Afrika 2013 kwa
kuifunga Burkina-faso 1-0.
Kabla ya AFCON 2013 Naija
ilikua kwenye nafasi ya 52 ambapo licha ya hivyo nchi hiyo imeendelea
kuwa nyuma ya Ivory Coast ambayo inabakia kuwa timu namba moja Afrika
huku ikishika nafasi ya 12 kidunia, Nigeria ni ya nne kwa Afrika.
Afrika kusini imepanda kwa
nafasi 25 zaidi kwenye viwango hivyo vya shirikisho la soka duniani
hivyo kufikia nafasi ya 60 kidunia.
Nchi ambazo zimeingia 10 bora
Afrika ni pamoja na Algeria, Tunisia, Zambia, Central African Republic,
Burkina Faso na South Afrika wakati timu 5 bora za dunia ni Hispania,
Ujerumani, Argentina, England na Italia.
Tanzania imeshuka kwa nafasi
tatu na sasa hivi inashika nafasi ya 127 pamoja na kwamba iliifunga
Cameroon 1-0 hivi karibuni ambapo kama haufahamu, nafasi kubwa kuwahi
kushikwa na Tanzania kwenye hivyo viwango ni 65 na hiyo ilikua mwaka
1995.
No comments:
Post a Comment