facebook likes

Thursday, February 28, 2013

HEADLINES ZA HABARI ZA MICHEZO DUNIANI.


.
RAFAEL BENITEZ VS JOHN TERRY
Nahodha wa Chelsea John Terry na kocha wa muda wa club hiyo Rafael Benitez wameripotiwa kuwa kwenye mzozo mkubwa kufuatia ugomvi ulioibuka kwenye kiwanja cha mazoezi cha club hiyo Cobham London.
Wawili hao walionekana kugombana baada ya Benitez kuitisha mkutano mdogo kabla ya mazoezi ya asubuhi ambao alizungumzia mechi yao ya jumapili waliyochapwa 2-0 na Man City.

LUIS NANI – Mchezaji winga wa Manchester United Luis Nani amepewa nafasi ya mwisho kusaini mkataba mpya na club yake wa mshahara wa pound elfu 90 ama ajiandae kuuzwa.

DAVID VILLA - Mshambuliaji wa Hispania na club ya Barcelona David Villa ambae amekuwa kwenye orodha ya wanaowaniwa na club ya Arsenal, ameambiwa na club yake kwamba hatolazimishwa kubakia Barca endapo hatokua tayari kuendelea kubaki kwenye club hiyo.
Viongozi wa Barca wamesema wangependa kuona mchezaji huyo anabakia kwenye club yao lakini hawamlazimishi kufanya hivyo endapo atakua na malengo ya kuhamia kwengine.

MESSI NA FABREGAS: – Kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas ambae sasa yuko Barcelona amesema mshambuliaji wa timu hiyo Lionel Messi bado ana uwezo mkubwa wa kuibeba club yake.
Fabregas amemtetea Messi ikiwa ni kauli ya kumjibu kiungo wa Madrid Jose Callejon ambae anasema alimshuhudia Messi akimdhihaki kwa maneno machafu kocha msaidizi wa Real Madrid Aitor Karanka.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...