Mmoja wa wasaidizi wake amethibitisha kifo cha Goldie kupitia page ya twitter ya Goldi kwa kusema ni kweli msanii huyo amefariki dunia usiku wa february 14 2013 muda mfupi tu baada ya kuwasili Lagos Nigeria, hali yake ya afya ilibadilika ghafla ikabidi apelekwe hospitali ambako hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.
Taarifa nyingine nilizozipata kutoka kwa mtu wake wa karibu wanaeshirikiana kimuziki zimeeleza kwamba mpenzi wake Goldie ambae ni Msanii wa Kenya CMB Prezzo ametua Nigeria usiku huu muda mfupi uliopita kwa ajili ya kuendeleza mipango aliyokua nayo na Goldie ikiwemo kutengeneza show ya TV.
Prezzo alitakiwa kushiriki katika TV show ambayo yeye na Goldie wangekua moja ya wahusika wakuu ambapo mpango ulikua baada ya mwezi mmoja Goldie na Prezzo wangekuja Tanzania, Uganda na Kenya kwa ajili ya kujitangaza na kuipromote single mpya ya Goldie ya ‘Skibobo’ aliyofanya na Ay.

Huyu
Deji ni mtangazaji wa Radio huko Nigeria ambae Goldie ndio
aliniunganisha nae, muda mfupi baada ya kupata taarifa za Goldie ilibini
nimtumie msg ili kujua kama ni kweli, na majibu yake ndio hayo hapo
juu.

No comments:
Post a Comment