facebook likes

Wednesday, July 17, 2013

Baada ya Jay Z na P.Diddy kufanya vizuri..rapper mwingine mkubwa aingia kwenye dunia ya fashion na brand ya nguo zake

Kama ulikua hujui mtu wangu wa nguvu chukua hii, lebo ya nguo Sean John ambayo inamilikiwa na P.Diddy inachangia kiasi kikubwa sana cha utajiri wa jamaa huyu ambaye kwa sasa amehamia kwenye Tv channel akiwa na channel yake inayoitwa Revolt. Rapper mwingine ambaye amefaidika sana na biashara ya mavazi ni Jay Z alivyokuwa anamiliki Roca Wear kabla hajaiuza. Rapper mwingine mkubwa ambaye kwa sasa yupo kwenye harakati za uwekezaji sana ni Nas. Hivi karibuni na ameanzisha lebo yake ya mavazi ya kiume na kuipa jina la HSTRY, kama ulikuwa haujapata story nyingine ya Nas ni kwamba yuko mbioni kufungua duka lake la sneakers pia. Kwenye brand yake ya mavazi Nas unaambiwa ameshiriki kwenye ku-design mavazi hayo ambayo yana material tofauti lakini ngozi imechukua nafasi kubwa sana hasa kwenye makoti. Tarehe moja mwezi wa nane ndiyo siku ambayo mavazi hayo yataingia sokoni.Hizi picha ni baadhi ya nguo za HSTRY ya Nas.


wenn33606711-e1332766608260
look4
look3
look2
look1
1

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...