
Chelsea imekuwa ikifuatilia hali ya Wayne Rooney ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu hivo karibuni huku mustakabali wake ukiwa haujapata ufumbuzi . Mshambuliaji huyo hapo jana aliripotiwa na magazeti ya huko England kukerwa na kauli ya kocha wake mpya David Moyes ambaye alisema kuwa Rooney atacheza kama mbadala wa mshambuliaji chaguo la kwanza Robin Van Persie .
Rooney kwa muda mrefu ameonyesha kutofurahishwa na kitendo cha kutopangwa kwenye nafasi anayoipenda ya ushambuliaji wa kati ambapo amekuwa akibadilishwa mara kwa mara kwenye nafasi tofauti kuanzia pembeni hadi nafasi ya kiungo cha kati.
Msimu uliopita Sir Alex Ferguson alitoa taarifa kuwa Wayne amemtaarifu kuwa anataka kuondoka , taarifa ambayo hata hivyo ilikanushwa baadaye . Hata hivyo David Moyes baada ya kusisitiza kuwa Rooney hatouzwa alionekana kwenda mbali kwa kauli aliyoitoa ambapo alisema kuwa hataruhusu mshambuliaji huyo kuonekana mkubwa kuliko klabu nzima ya United.
No comments:
Post a Comment