Vita dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya ni ya dunia nzima ambapo kila nchi inafanya kila liwezekanalo kutafuta vyanzo vya mitandao mikubwa inayofanya biashara hiyo. Serikali ya Mexico imefanikiwa kumkamata kiongozi wa mtandao mkubwa wa matukio ya kihalifu na usambazaji wa dawa za kulevya nchini humo unaofahamika kama ‘Zest’ aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba Taarifa iliyoripotiwa na Reuters inasema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina la Miguel Angel Trevino aka Z-40, alifanikiwa kukamatwa jana (July 15) baada ya askari kuifuatilia gari yake ya Pickup kwa helicopter.
Msemaji wa serikali ya Mexico Eduardo Sanchez amesema, Trevino ( 40), alikamatwa akiwa na washirika wake wengine wawili kufuatia operesheni ya miezi mingi ya kumsaka, na alikutwa akiwa na pesa taslim zaidi ya $2 million.
Kukamatwa kwa Z-40 ni ushindi mkubwa kwa serikali ya Mexico kutokana na ukubwa wa mtandao huo wa Zetas ambao umekua tishio nchini humo kutokana na vitendo vya matukio ya mauaji yaliyofanywa na magenge ya mtandao huo unaojihusisha pia na biashara haramu ya dawa za kulevya, vitendo ambavyo vimechafua jina la nchi hiyo kiasi cha kuwapa hofu watalii na wawekezaji.
No comments:
Post a Comment