Msanii Young Dee amekanusha uvumi
ulioenea mitaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na
kusema kuwa pamoja na story hizo kuwa kubwa lakini hali hiyo
haijamuathiri sana kwasababu hazina ukweli wowote.
“Ni story ambazo zimekuwa kubwa
sana lakini hazijaniathiri sana kwasababu sio ukweli, lakini zimenifanya
nimezidi kuwa makini sana kuwa muoga pia na vitu vingi sana kuangalia
watu wanaonizunguka, mazingira na vitu kama hivyo”.
Alisema Young Dar es salaam kupitia E-News ya EATV jana .
Dee amesema kuwa anafahamu fika kuwa
utumiaji wa ‘unga’ unaweza kuathiri kazi yake ya muziki kutokana na
mifano hai ambayo imeshaonekana kwa wasanii wengine,
“The more the story zinakuwa kubwa
zinapoteza maana nzima ya kitu nachohangaikia kila siku ambayo ni
muziki, so naonekana muziki nafanya nakula unga na mifano ipo watu ambao
wameingia kitika hayo mambo”.
Young Dee alimaliza kwa kusema kama kweli maneno yanayosemwa mtaani yana ukweli basi watu watagundua haraka,
“mi ambacho naweza kusema unga hauna siri haufichiki so kama mi nakula unga people they can easily notice haraka sana”.
No comments:
Post a Comment