facebook likes

Monday, October 7, 2013

MZEE ZAHIR ZORRO KUWA JUDGE WA TUSKER PROJECT FAME SEASON 6

Muimbaji mkongwe wa muziki Tanzania, Zahir Ali Zorro ameungana na Ian Mbugua wa Kenya na muimbaji Juliana Kanyomozi wa Uganda kama majaji wa Tusker Project Fame, msimu wa 6.
IMG_4219
SOMA ZAIDI....
“Tanzanian music legend Zahir Ali Zoro joins the #TPF6 judging team. He’ll be one of the judges alongside @IanMbugua and @JKanyomozi,” kimeandika kituo cha runingo cha Citizen TV cha Kenya kinachorusha mashindano hayo. Zahir Zorro ni baba mzazi wa wanamuziki Banana na Maunda Zorro. Mwanamuziki huyo mkongwe amechukua nafasi ya Hermes Lyimo aka Hermy B aliyekuwa jaji kwa misimu kadhaa ya shindano hilo. Hata hivyo, kuchukuliwa kwa Zorro kama jaji wa shindano hilo, kumepokelewa kwa hisia tofauti huku wengi wakionesha kutomkubali. Hizi ni baadhi ta tweets kumhusu #JudgeZorro. Hata hivyo si wote wanaomdhihaki: 

Source: Bongo5

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...