
Raha ya mechi bao: Michu akienda kwa Jonjo Shelvey (kulia) kushangilia naye baada ya kuifungia bao la pili Swansea dakika ya 64 ikimenyana na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana. SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI....Timu hizo zilitoka 2-2 bao lingine la Swansea likifungwa na Jonjo dakika ya pili tu, wakati mabao ya Liverpool yalifungwa na Sturridge dakika ya nne na Moses dakika ya 36.

Kazi nzuri: Michu akishangilia baada ya kuifungia Swansea bao la pili

Shujaa: Jonjo Shelvey akishangilia baada ya kuifungia Swansea bao la kwanza


Kitu hicho: Shelvey akifumua shuti kufunga

Heshima: Steven Gerrard alivaa beji ya Unahodha Liverpool kwa mara ya 400

Babu kubwa: Shelvey akileta kizaazaa langoni mwa Liverpool

Mimi tena: Daniel Sturridge akiifungia bao la kusawazisha Liverpool, baada ya Shelvey kuifungia la kwanza Swansea


Anawarudisha kati: Wa mkopo kutoka Chelsea, Victor Moses amefunga katika mechi yake ya kwanza Liverpool

Jaribio zuri: Coutinho (kushoto) akibinuka tik tak mbele ya Wilfried Bony (kulia)

Kiulaini: Michu akifunga

No comments:
Post a Comment