Jumatatu ijayo ni siku maalum sana kwa bondia Francis Cheka aliyeitoa kimasomaso Tanzania hivi karibuni baada ya kumtwanga kwa pointi Mmarekani Phill Williams 'The Drill' na kutwaa ubingwa wa WBF uzito wa kati.
SOMA ZAIDI......Cheka, ataanza rasmi pre-form one katika shule ya St. Joseph huko Morogoro, akisomea masomo ya Kiingereza na Biashara.
Akizungumzia hilo, Cheka amesema "Sikupata elimu nzuri nikiwa mdogo kutokana na matatizo ya kifamilia, lakini sasa nitaitumia nafasi hii kujiendeleza zaidi. Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali zaidi, hadi namaliza miaka 10 kwenye masomo yangu nitakuwa na miaka 41 hivyo naweza kuamua kama niendelee na ngumi au nifanye kazi nyingine"
Cheka alijiunga kwenye ngumi za kulipwa mwaka 2000 akitokjea kwenye ngumi za ridhaa na kufanikiwa kutwaa mikanda ya WBC, IBF afrika, UBO, IBU, WBO, WBF na ubingwa wa Taifa.
Nini maoni yako kuhusu uamuzi wa Cheka?
source- allanluckyblog
No comments:
Post a Comment