facebook likes

Sunday, September 8, 2013

Fally avunja rekodi!!

Mwanamuziki wa kizazi cha tano cha muziki wa Congo Fally Ipupa kwa sasa ndiye Mwanamuziki anayeongoza kwa kuwa na Show nyingi kuliko wote.

 SOMA ZAIDI..........

Habari zinasema toka aanze shughuli za muziki akiwa kama solo artist, Fally Ipupa kwa mwaka huu hajawahi kukaa Congo zaidi ya Wiki bila kupata mualiko ama ndani ya nchi ama nje ya nchi, Majuzi Fally Ipupa ametoka nchini Amerika ambako alikwenda kwa ajili ya kufanya shooting ya Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake mya ya Power ambapo amemshirikisha mwanamuziki R.Kelly humo ndani.
Wiki hii tarehe 6 September mwanamuziki Fally Ipupa atakuwa na show ya kufa mtu itakayofanyika katika ukumbi wa bwawa la hoteli ya Grand Hotel huko Kinshasa onyesho lililopewa jina la Power.


Fally amechukua Tuzo za uandishi na tungo zake mara tatu za Droit chemin ,Arsenal de belles mélodies et Power, kosa, leka, hii imemfanya aweze kuwa na maonyesho mengi ndani na nje ya nchi, sababu ya pili ni kuwa Fally hafungamani na upande wowote kwenye siasa za Congo jambo linalompa nafasi ya kupata mialiko ndani na nje ya Congo hasa Ufaransa na Ubelgiji ambako kuna Wacongoman wengi na mashabiki wengi wa muziki huu wa DRC.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...