facebook likes

Friday, September 27, 2013

Ajali ya malori manne yaua watu watatu


Watu watatu wamekufa papo hapo kufuatia ajali mbaya iliyotokea katika Mlima Inyara wilayani Mbeya ikihusisha malori manne, mawili kati yake kugongana uso kwa uso yakiwa kwenye mwendo mkali na kisha kulipuka moto ulioteketeza mengine.
SOMA NA ANGALIA PICHA ZAIDI...
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1:30 asubuhi kwenye mtelemko mkali wa mlima Inyara.
Walioshuhudia walisema chanzo ni lori lililokuwa limebeba shehena ya shaba, likitokea Zambia kwenda Dar es Salaam, kujaribu kulipita lori lingine ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara na ndipo lilipogongana uso kwa uso na lori la mafuta ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda DRC Kongo.
Kwa mujibu wa mahuhuda hao, baada ya malori hayo kugongana uso kwa uso lori la mafuta lilipuka moto ambao ulienea katika eneo hilo lote na kuteketeza lori la mafuta na sehemu kubwa ya magari mengine.

Huruma Daniel alisema akiwa nyumbani kwake alisikia kishindo kikubwa barabarani na alipoangalia aliona moto mkubwa ukiteketeza magari barabani na alipofika kwenye eneo la tukio alikuta watu watatu waliokuwa ndani ya malori wakiwa wamekufa na ndipo aliposhirikiana na wenzake kuitoa miili kutoka kwenye magari.
Alisema baada ya muda mfupi askari wa Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji walifika katika eneo hilo na kuichukua miili ya marehemu.

Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, Coplo Athuman Mwasile, alisema baada ya kufika kwenye eneo la tukio walikuta moto mkali ukiendelea kuwaka na ndipo walipouzima na kuitoa miili ya watu wawili katika lori mojawapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, aliyataja magari yaliyopata ajali kuwa ni lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 605 AXX lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 480 CAX lililokuwa likitokea nchini Zambia kwenda Dar es Salaam.
Alisema kuwa lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Wilson Chacha akiwa na utingo wake, Juma Salehe wakazi wa Jijini Dar es Salaam na wote walikufa papo hapo na kuwa lori hilo liligonga kwa nyuma lori lingine namba T 548 BLY lililokuwa na tela ambalo lilikuwa likiendeshwa na Samweli Aron (30) mkazi wa Sinza, jijini Dar es Salaam na kusababisha gari hilo kuligonga lori lingine lililokuwa na tela ambalo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara.
Alisema lori namba za usajili T.605 AXX na tela lake lilipoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari lingine T 225 AKV likiwa na tela kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya Mjini.

Baada ya magari hayo kugongana, mto mkubwa ulilipuka na kusababisha mwili wa dereva Sixtus kuteketea kabisa.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...