facebook likes

Saturday, July 20, 2013

Unaionaje hii…shindano la kupunguza uzito na mshindi kupata dhahabu yenye thamani zaidi ya millioni 8


To match feature GOLD-FIXING/
Kutokana na hali ya watu kunenepa ovyo kwasababu ya aina maisha wanayoishi hasa kwenye vyakula wanavyokula. Halmashauri ya
jiji kubwa duniani “Dubai”, limenzisha kampeni waliyoipa jina la “Your Weight in Gold”. Unaambiwa kwa kila kilo moja utakayopunguza unapata 1gm ya pure gold.
Mchakato huo unahusisha watu watakao punguza kilo zaidi ya mbili ndani ya siku 30. Lakini kwa watu watatu watakao punguza zaidi uzito wao, watapata nafasi ya kushinda kiasi cha dhahabu chenye thamani zaidi ya millioni 8 (Dh20,000). Mtu wangu wa nguvu hili shindano lingekuwa hapa Dar mambo yangekuwaje?, watu wangu wauza chips na wauzaji wengine wa vyakula soko lingepungua huku watu wakijitahidi kuzipa hizo dhahabu kwa kupunguza kura na kufanya mazoezi yakutosha.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...