KALI YA LEO: JOSE MOURINHO AJICHORA TATTOO YA JINA LA MKE WAKE MKONONI MWAKE
Boss wa CHELSEA Jose Mourinho amefanya kitendo ambacho sio watu wengi
wenye umri wake wanaweza kufanya - mreno huyo amechora tattoo yenye la
mkewe kwenye mkono wake.
Mourinho, mwenye miaka 50, alijichora tattoo hiyo baada ya kurejea na timu yake kutoka mashariki ya mbali. Alilipa kiasi cha £80 ili kuchora jina la mkewe 'Matilde Faria' baada ya kuvutiwa na michoro aliyoiona kwa mmoja wa wafanyakazi wa klabu ya Chelsea.
Kocha huyo mwenye majivuno alitumia saa nzima kutulia na kuchorwa tattoo
hiyo ambayo ndio ya kwanza kwa mchoraji anayefanya shughuli zake karibu
na uwanja wa Chelsea uliopo magharibi mwa London.
Mtu aliyemshuhudia kocha alikaririwa akisema kwamba: “Jose alionekana mtu mwenye furaha baada ya kuchora tattoo hiyo.”
No comments:
Post a Comment