HUKU
zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Wazi la
Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’
ambalo litafanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza, maandalizi
yake yamezidi kupamba moto.
Mratibu
wa Tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa
Kissoky, alisema kwa sasa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni
kuanza kwa tamasha hilo Jumatatu ijayo.
Kissoky
alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na
kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani
vitu vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida. “Kwa
sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu
tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa
na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
Naye
Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha
hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani
wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. “Tumejipanga
katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa
Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi .
Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania
kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,”
alisema Consolata.
Naye
Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na
ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake
na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa. “Tumeona
jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo
Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa
ana, sasa kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.
Tamasha
la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku
kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu
zote hizo ni kutoka Tanzania.Wasanii
wakali wa Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’,
Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk
Cheni’na Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii walioahidi kufanya
kweli pia katika tamasha hilo.
Tamasha
hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na
kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL).
No comments:
Post a Comment