Kaimu
Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi
wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity .
Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia
kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro
unao endelea Chuoni hapo
***************
HALI
si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya
Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake
kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani
ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai
Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo
huo umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye
katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo
hicho kilichopo Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na
kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye
amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo
ambazo Menejimenti ya Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha
mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo
ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi
yanayohusu Taaluma.
Kwa
taarifa zaidi na madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga
mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu
yameandikwa kwenye barua hapo chini lakini habari kamili itawajia
baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.
No comments:
Post a Comment