facebook likes

Saturday, February 23, 2013

PREZZO AREJEA KENYA
































Rapa Jackson Makini ama Prezzo ametua nchini Kenya baada ya kukaa kwa wiki moja mjini Lagos, Nigeria alipokuwa amekwenda kwa ajili ya kufurahia siku ya wapendanao yaani Valentines Day ambapo badala yake akakutana na msiba mzito baada ya kifo cha mpenzi wake Goldie katika siku hiyo muhimu.
Prezzo ambaye hakutaka kufanya aina yeyote ya mahojiano imemlazimu kurudi nchini Kenya baada ya familia ya marehemu Goldie kutokuwa na taarifa kamili juu ya mipango ya mazishi ya mpendwa wao Goldie Harvey.

Aidha watu wa karibu wa rapa Prezzo wamethibitisha uwepo wake akiungana na ndugu wa marehemu katika uombolezaji tofauti na bwana wa marehemu Andrew Harvey ambae kila kukicha alikuwa bize akifanya mahojiano na vyombo vya habari ambapo taarifa zilizopo ni kwamba yupo
nchini Uingereza.


No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...