Unaambiwa stori za kuaminika 
zinatiririsha kwamba mwimbaji star wa dunia Beyonce amekataa kabisa 
kuonana na mdogo wake wa kiume aitwae Nixon (3) ambae baba mzazi wa 
Beyonce amempata na mwanamke mwingine wa nje ya ndoa aitwae Alexandra 
Wright.
Hiyo ni moja ya sababu kuu 
ambazo inadaiwa ndio zilivunja uhusiano kati ya mzee Knowles na mama 
Knowles pamoja na kina Beyonce huku za kuaminika zikipasha zaidi kwamba 
ndio kilikua chanzo cha Beyonce pia kujiondoa kuwa chini ya baba yake 
kikazi manake mwanzoni Knowles ndio alikua meneja wa Beyonce.
The Box wameripoti pia kwamba 
uhusiano wa mzee Knowles na Alexandra ndio uliivunja ndoa yake na Tina 
ambae ndio mama mzazi wa Beyonce ambapo star Magazine wameripoti tena 
kwamba Beyonce hana furaha na baba yake sasa hivi kwa hiyo dhambi 
aliyofanya baada ya ndoa yake kudumu kwa miaka 31.
Pamoja na kwamba mzee Knowles 
aliamua kuhamia kwa nyumba ndogo na kuamua kuzaa mtoto mmoja, mke wa 
nyumba ndogo ambae ni Alexandra amesema uhusiano wake na Knowles ulikua 
wa miezi 18 tu ambayo waliishi pamoja ila baada ya hapo mzee akaanza 
kuzingua wakati Alexandra akiwa mjamzito na hata alipojifungua mzee 
akamtelekeza.
Pamoja na kwamba mzee huyu 
alimkataa huyu mtoto wa nje, vipimo vilionyesha kwamba mtoto ni wake 
kabisa ambapo Mahakama moja Los Angeles Marekani ilimuamuru atoe dola 
elfu 8,200 kama matunzo ya mtoto.
Mzee Knowles ni mmoja kati ya 
wenye heshima kwenye muziki, ndio mtu aliyegundua kipaji cha Beyonce na 
hata kuunda kundi la Destiny’s Child, one of the biggest girl groups of 
all time.
Beyonce sio staa wa kwanza 
kusikia kwamba hapatani au haongei na baba yake, imeshatokea kwa Kelly 
Rowland pia na hata movie star ambae amewahi kuja Tanzania kwenye mbuga 
za wanyama na kulala kwenye hoteli namba moja duniani Angelina Jolie.



No comments:
Post a Comment