Siku ya Jumatatu serikali ya Uganda iliwasimamisha wanajeshi 24 wanaohudumu kwenye Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kwa tuhuma za kuuza chakula na mafuta kilichokusudiwa wanajeshi wa Uganda kwa njia ya magendo.
Kamanda wa kikosi cha Uganda, Brigedia Michael Ondoga, alikuwa miongoni mwa walioitwa nyumbani na Rais Yoweri Museveni, ambaye pia alifuta uteuzi mpya wa Ondoga kama mwambata wa kijeshi katika balozi jijini Nairobi, liliripoti gazeti la Daily Monitor la Uganda.
Wanajeshi wa Uganda waliopelekwa kama walinda amani nchini Somalia walikuwa kila mara wakila mlo mmoja tu kwa siku kwa sababu ya kashfa hiyo, uchunguzi wa gazeti hilo ulibainisha mwezi Juni.
Wanajeshi waliosimamishwa kazi walitarajiwa kurudi Uganda siku ya jana kukabiliana na kesi kwenye mahakama ya kijeshi.
source:djsek
No comments:
Post a Comment