facebook likes

Sunday, August 4, 2013

Real Madrid yaongeza dau kwa Bale,sasa ni pauni milioni 100.


Real Madrid yaongeza dau kwa Bale,sasa ni pauni milioni 100.
Kocha wa Real Madrid,Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa mazungumzo yao dhidi ya klabu ya Tottenham juu ya kumsajili Gareth Bale yanaendelea vizuri na sasa wameamua kuongeza dau na kufikia pauni milioni 100.
Muitaliano huyo amesema kuwa Alhamisi walianza mazungumzo rasmi na klabu hiyo ya London ili  kufanya biashara ya kumnunua nyota huyo raia wa Wales,ambaye alimwambia kocha wake Andre Villas-Boas kuwa angependa kuondoka klabuni hapo.
Madrid wapo tayari kutoa kiasi hicho kikubwa cha pesa na kuvunja rekodi ya dunia ya usajili wa kiasi cha pauni milioni 80 ambacho walikitoa kwa Cristiano Ronaldo walipomnunua kutoka Manchester United mwaka 2009 .
Ancelotti aliendelea kusema kuwa wanasubiri kuona nini kitatokea kwani kwa sasa mazungumzo yapo baina ya klabu hizo mbili,huku akidai kuwa timu yao ipo imara na wapo tayari kuona maendeleo yao ya baadae yatakuwaje.
Ancelotti

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...