facebook likes

Tuesday, August 20, 2013

HABARI NJEMA: WAZAZI WA MTOTO MANKA ALIYEOKOTWA JANA UPANGA WAPATIKANA


Globu ya Jamii ina furaha na fahari kutangaza kwamba hatimaye wazazi wa mtoto wa kike Manka wamepatikana na tayari wamemchukua binti yao tokea jana usiku.
SOMA ZAIDI......
Manka, mwenye umri kati ya miaka 3-4 ambaye jana jioni tulimtangaza kuwa ameokotwa maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kuhifadhiwa kituo kidogo cha Polisi cha Salender, ameungana na wazazi wake ambao waliiona taarifa hii mara moja.
Msamaria mwema aliyetuma habari hii anasema amefurahi sana wazazi wa Manka kupatikana kwani kama mzazi alijihisi vibaya sana kuona mtoto kapotea. Anawashukuru pia askari wa kituo cha Salender kwa kufanikisha hilo. Anamtakia Manka maisha mema na ya fanaka.

No comments:

COMMENTS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...