Taarifa ikufikie kwamba baada
ya watu wengi kuwa na hamu ya kufahamu ni lini David Beckam atacheza
mechi yake ya kwanza toka ajiunge na club ya PSG ya Ufaransa, jibu
limetoka tayari.
Alielitoa ni kocha Ancelotti
kwamba Beckham ataingia uwanjani kwa mara ya kwanza akiwa na PSG kwenye
mechi dhidi ya Marseille siku ya jumapili.
Marseille iko nafasi ya tatu pointi 5 nyuma ya PSG ambapo kwenye hiyo mechi club hii itamkosa striker Jordan Ayew ambae ana suspension na pia midfielder Benoit Cheyrou ambae ni majeruhi.
No comments:
Post a Comment