Askofu mkuu wa Canterbury
amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa Benedict wa XVI kwa
huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake, kiongozi wa
Ujeremani Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala
wa makanisa, waislamu na wayahudi.
Kasema uamuzi na hatua ya Papa
Benedict XVI kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya takriban miaka
minane kuliongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni
mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo, ni
sahihi
Makao makuu ya Kanisa Katoliki
huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya atachaguliwa kabla ya mwisho
wa mwezi wa tatu na sherehe za Pasaka ambapo kama hufahamu, tabia ya
kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni tukio jipya katika karne za hivi
karibuni.
Mwandishi wa BBC Roma Alan
Johnston anasema habari hizi zimetokea kama radi, hakukua natetesi
yoyote juu ya uwezekano kama huu na hata msemaji wa Vatican Father
Federico Lombardi amesema hata wasaidizi wa Papa wa karibu mno hawakuwa
na fununu juu ya tukio hili.
Kaka yake Papa akizungumza
kutoka nyumbani kwake huko Regensburg Ujerumani, Georg Ratzinger amesema
Papa alikuwa ameanza kupata shida kutembea.
Wakati wa kutawazwa kama Papa,
Kadinali Joseph Ratzinger alikuwa mmojawapo wa mapapa wapya kuchaliwa
akiwa mwenye na umri mkubwa wa miaka 78 na alitangazwa kuwa Papa Aprili
2005 kufuatia kifo cha marehemu John Paul wa pili.
Uongozi wake ulitokea wakati wa
wimbi kali la ubakaji kulikumba kanisa katoliki katika kipindi cha
miongo mingi, ubakaji uliofanywa na watawa dhidi ya watoto wavulana
ambapo Papa amekaririwa akisema “baada ya kujichunguza binafsi na nafsi
yangu mbele ya Mola wangu, nimefikia uwamuzi kua uwezo wangu na afya,
ukiambatana na umri mkubwa, ni mambo yatakayokwaza jitihada zangu za
kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki”
Kwa mujibu wa BBC Swahili
walioiandaa hii ripoti, Kuna kipengele katika sheria ya Kanisa
kinachosema kuwa kujiuzulu kwa Papa kunakubalika iwapo kitendo hicho
kimefanywa kwa hiari na kwa utaratibu unaostahiki.
No comments:
Post a Comment