BARABARA YA OLD BAGAMOYO SASA KUITWA MWAI KIBAKI
Barabara
iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Old Bagamoyo kuanzia leo itaanza
kuitwa jina la 'Mwai Kibaki road' ikiwa ni heshima kwa aliyotunukiwa
rais huyo wa Kenya kwa ziara yake ya siku mbili nchini hapa.
Mkuu mkoa wa Dar es salaam Meck Sadik amesema barabara hiyo yenye urefu
wa Km 10.1 ni kuanzia kwenye mataa ya Morocco hadi mzunguko wa kuelekea
Africa Mbezi beach mkabala na uwanja wa JWTZ.
Pia Rais Mwai Kibaki atatumia fursa hiyo kuwaaga na kuwashukuru
watanzania kwa ushirikiano wao kipindi cha uongozi wake maana muhula wa
uongozi wake unaelekea kikomo hapo baadaye mwaka huu.
No comments:
Post a Comment