Wizara ya elimu na mafunzo ya
ufundi february 18 2013 imetangaza matokeo ya kidato cha nne 2012 ambapo
yameonyesha kiwango cha kufaulu kimeshuka kwa asilimia kubwa
ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Waziri wa wizara hiyo Dr.
Shukuru Kawambwa amesema kati ya wanafunzi laki nne na elfu 56
waliofanya mtihani, wanafunzi laki mbili na elfu 40 sawa na nusu ya wote
waliofanya mtihani, wamefeli kwa kupata sifuri ambapo pia matokeo
yameonyesha shule binafsi zimeendelea kufanya vizuri ikilinganishwa na
shule za serikali huku idadi ya kufaulu kwa daraja la kwanza hadi la
tatu nayo ikishuka kwa zaidi ya asilimi 50.
Namkariri Dr Kawambwa akisema
“Tathmini ya awali iliyofanywa kuhusu ufaulu wa Watahiniwa katika shule
mbalimbali inaonyesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo
zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu
iliyokamilika, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha, shule
zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kukosa walimu wa sayansi na hisabati kwa shule za
vijijini, kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mkondo wa sayansi na
kutokuwepo kwa maabara kwa ajili ya kujisomea”
Waliopata division 1 ni
wavulana elfu moja na sabini na tatu, wasichana ni mia tano 68 ambapo
jumla yao ni 1641, division two wavulana ni elfu 4 mia 4 na 56 na
wasichana ni elfu 1 mia 9 na 97 jumla yao ni elfu 6453, division three
wavulana na elfu 10 mia 8 na 13 na wasichana ni elfu 4 mia 6 na 13 jumla
yao ni elfu 15 mia 4 na 26, ukijumlisha divisio one mpaka three wavulana ni 16342 na wasichana 7178.
Katika mtihani huo jumla ya
wanafunzi 728 wamefutiwa majibu ya mtihani wao kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo ya udanganyifu pamoja na kutoa lugha chafu.
No comments:
Post a Comment