Sehemu ya dawa zilizokama twa katka Operesheni.
Wadau wa habari wakifuatil
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ) imekamata dawa bandia zenye thamani ya TSh. 49,634,733/= katika operesheni maalum ijulikanayo kama Operesheni GIBOIA iliyoshirikisha Jeshi la Polisi nchini, Shirikisho la Polisi la Kimataifa (Interpol), Baraza la Famasi, TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Viwango (TBS), Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Rais na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Operesheni GIBOIA ilifanyika kuanzia tarehe 1-3 Oktoba, 2013 katika mikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma na Dar es Salaam. Operesheni hii pia imefanyika sanjari katika nchi saba zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo ni Afrika ya Kusini, Angola, Malawi, Msumbiji, Swaziland, Zambia na Tanzania kwa lengo la kupambana na dawa Bandia Barani Afrika.
No comments:
Post a Comment